Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.NOV 11.2016 SAA 01:11 USIKU
Ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 za klabu zote za Ligi
Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza Novemba 15, 2016 kwa
mchezo maalumu wa
ufunguzi utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
linachukua nafasi hii kuzikumbusha klabu kuwa zina taarifa kuhusu kuwako
kwa ligi hiyo ya U20 na kwamba mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni
Novemba 3, mwaka huu katika barua maalumu kwa kila klabu yenye Kumb. Na.
TPLB/CEO/2016/036.
Tayari klabu hizo zimepewa shilingi milioni 10 (Sh
10,000,000) kutokana na udhamini wa Benki ya DTB kwa ajili ya kushiriki
michuano hiyo. Pia kila klabu itapewa shilingi milioni 10 (Sh
10,000,000) nyingine kutokana na udhamini wa matangazo ya ligi ya U20 wa
Azam Tv.
Kwa udhamini huo kila klabu itajigharimia usafiri
wa kwenda na kurudi kituoni, malazi, na chakula kwa kipindi chote cha
mashindano. Vituo vilivyopangwa ni Dar es Salaan ambako kuna timu za JKT
Ruvu, Simba, Ruvu Shooting, Ndanda, Majimaji ya Songea, Mtibwa, Mbeya
City na Tanzania Prisons.
Kituo kingine ni Bukoba mkoani Kagera ambako kuna
timu za Azam, African Lyon, Mbao FC, Toto Africans, Mwadui ya Shinyanga
kama ilivyo Stand United, Kagera Sugar na Young Africans ambazo
zitafungua dimba hiyo Novemba 15 kwa mchezo pekee.
Tunazikumbusha klabu kuzingatia Kanuni ya 42 (27)
ya Ligi Kuu ya Vodacom inayosema: “Klabu ambayo haikupeleka uwanjani
timu ya U20, mechi ya kwanza itapigwa faini ya Sh 2,000,000 na
kunyang’anywa na kupoteza mchezo, mechi ya pili itapigwa faini ya Sh
2,000,000 na kunyang’anywa pointi tatu katika Ligi ya Wakubwa (Ligi Kuu)
na Ligi ya Wadogo (u20).
Pia
tunazikumbusha klabu kuwa kwa mujibu wa Kanuni, wachezaji saba (7)
kutoka U17 wanaruhusiwa kuchezea timu ya U20. Ruhusa hiyo ni kwa
wachezaji wa U17 waliosajiliwa, kwa maana kuwa katika ligi zote
wachezaji wanatambuliwa kwa kutumia leseni.
0 Comments