Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.NOV 11.2016 SAA 12:38 JIONI
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Wanawake ‘Twiga
Stars’ jana Novemba 10, 2016 ilipoteza kwa taabu mchezo wake wa kwanza
wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji Cameroon ambayo ilipata
mtihani mzito kwa Watanzania kwa dakika zote kabla ya kuibuka kwa
ushindi wa mabao 2-0.
Cameroon ambayo ilijipanga kushinda mabao mengi,
ilitolewa jasho na hivyo kuomba mchezo mwingine ambao sasa utafanyika
Jumapili Novemba 13, mwaka huu jijini Yaounde na Kocha Mkuu wa Twiga
Stars, Sebastian Nkoma amesema: “Nimeona upungufu katika mchezo wa jana,
nafanyia kazi.”
Bao la kwanza katika mchezo wa jana lilifungwa na
Mshambuliaji Ngoya Ajara wa Klabu ya Sundsvalls ya Sweden ambaye pia
ndiye Mchezaji Bora wa mwaka 2016 nchini Cameroon wakati bao la pili
lilifungwa na Kiungo wa Klabu ya Aurillac ya Ufaransa Ngono Mani
Michelle katika dakika ya 71.
Twiga Stars wao wamealikwa na Waandaaji wa fainali
za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016 – Cameroon ambao
wameamua kuipa heshima Tanzania na kuona kuwa timu hiyo ina ubora wa na
kwamba inafaa kuipimana ubavu kabla ya kuanza kwa fainali hizo Novemba
19, mwaka huu.
Twiga Stars ambayo sehemu kubwa ya kikosi hicho
kinaundwa na wachezaji wa timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara
yaani Kilimanjaro Queens ina rekodi nzuri ya kuwa kinara wa viwango vya
ubora kwa nchi za Afrika Mashariki na kati lakini zaidi ni mabingwa
wapya wa ukanda huo – ubingwa uliopatikana Septemba, mwaka huu huko
Uganda.
Rekodi hizo zimesukuma Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon (FECAFOOT)
– nyumbani kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou kuikubali Twiga Stars na hivyo
kuomba kucheza nayo mwishoni mwa wiki hii. Tayari Twiga Stars imeanza
maandalizi ya kutosha chini ya Makocha Sebastian Nkoma na Wasaidizi wake
Edna Lema na El Uterry Mohrery.
Kikosi cha Twiga Stars wamo makipa, Fatma Omari na
Najiat Abbas; mabeki ni Wema Richard, Sophia Mwasikili, Anastasia
Katunzi, Maimuna Hamisi, Fatuma Issa, Happiness Mwaipaja na Mary Masatu
wakati viungo ni Donisia Minja, Stumai Abdallah, Amina Ally, Anna
Mwaisura na Fadila Kigarawa ilhali washambuliaji ni Fatuma Swalehe, Asha
Rashid na Mwanahamisi Omari.
Wakati huo huo, taarifa kutoka zinasema timu ya
taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’
imefungwa bao 1-0 na Seongnam katika mchezo wa kwanza wa kuwania Kombe
la Korea Kusini katika michuano iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa
Miguu la Korea Kusini. Mchezo huo ulifanyika jijini Seoul, Korea Kusini
na goli moja lililofungwa kipindi cha kwanza, vijana wetu wameonesha
uwezo mkubwa sana.
Kikosi kilicho anza ni Ramadhani Kabwili (1),
Kibwana Ally (12), Nickson Kibabage (3), Ally Msengi (14), Dickson Job
(5), Ally Ng'azi (2), Shaban Zubeir (13), Asad Juma (10), Mohamed Rshid
(11), Nashon Kelvin (7), na Muhsin Makame (19). Kipindi cha pili benchi
la Ufundi lilifanya mabadiliko aliingia Cyprian Mtesi (8) Kuchukua
nafasi ya Muhsin Mkame (2) na Errick Nkosi (4) kuchukua nafasi ya Ally
Ng'anzi (2).
0 Comments