Ticker

6/recent/ticker-posts

MKWASA AWAOMBA RADHI WATANZANIA,AWAPONGEZA WACHEZAJI KWA KUJITUMA

  Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.06,2016 SAA 08:08 MCHANA
Kocha Mkuu  wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa Ameomba radhi watanzania na na wanamichezo kwa
ujumla, kwa kutolewa katika mashindano Yya kufudhu michuano ya Afrika.

Taifa Stars ilicheza mechi siku ya Jumamosi Septemba 3, 2016 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017). Katika mchezo huo ambao mashabiki waliingia bure, Taifa Stars ilifungwa bao 1-0 mara baada ya kuibana Super Eagles hivyo kumsukuma Gavana huyo kuandaa hafla ya chakula cha jioni ambako mbali ya kuizawadia Stars, pia aliizawadia Super Eagles dola 35,000 za Marekani.
 
Katika Mkutano wake na waandishi wa habari hii Leo Mkwasa Amesema wachezaji wa Tanzania wamejitahidi katika mchezo huo  lakini hawakupata matokeo mazuri.

"Yale waliyotarajia yamekuwa tofauti,Nigeria ni timu kubwa walipereka kikosi  cha uhakika,Tanzania ilikuwa na wachezaji wageni lakini walicheza kadri walivyoelekezwa,wachezaji walicheza kwabidii na kutumikia nafasi kama walivyopewa majukumu".alisema mkwasa

Mkwasa pia a kipa metioa Shukrani kwa kipa Aishi Manura kwa kiwango kikibwa alichokionesha ,lakini pia amewapongeza wachezaji wengine kama Visenti Endru,David Mwantika na Shabalala kwa kuonesha pia kiwango kizuri katika mchezo huo.

Mkwasa Pia amesema wanahitaji muda wa maandalizi ili kuweza kumtumia Vizuri Mbwana Samatta,ameongeza kuwa timu nyingine zinakuwa tayari zimeshajuana na kuweza kuelewana.

"Maandalizi ni ya kuunga unga,kwa levo ya wachezaji wetu tunahitaji muda mzuri wa maandalizi na kuangalia jinsi ya kuwajenga wachezaji wetu,lazima wafanye mazoezi yakutosha ya kuwafanya kuwa na nguvu".

PiA Mkwasa ameliomba shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liwaandikie  barua wale wale waliopewa jukummu la kuwasafirisha kwenda Nigeria yaani shirika la ndege la Ethiopia,kwa kuwafanya wachezaji baadhi ya wachezaji waliotangulia nchini Ethiopia kuchoka mapema kwani mkwasa anasema walilala katika mabenchi ya uwanja wa ndege bila kuwapa mahitaji muhimu.

 Charles Boniface Mkwasa pia amezungumzia Swala la Program na kusema inatakiwa ziwe zinaheshimika,kwani Program zinatengenezwa lakini halitekelezwi,na kusisitiza kuwa TFF inatakiwa itambue kuwa ukishindwa kujiandaa basi unajiandaa kushindwa.

Swala la mchezaji Kelvin Yondani,mkwasa anasema kunahitajika kuangalia maslai ya mchezeji,lakini mchezaji huyo anatakiwa atambue umuhimu wake  na Uzalendo katika Timu ya Taifa,lakini amesisitiza yeye kama kocha hawezi kumpa adhibu yeyote kwa kile alichokifanya.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)


Post a Comment

0 Comments