Ticker

6/recent/ticker-posts

KUWAONA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI NI BUKU 7,000 TU,TFF YATOA UTARATIBU

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.27,2016 SAA 06:46 MCHANA
Maandalizi ya mchezo wa Simba na Yanga utakaopigwa jumamosi hii katika uewanja wa Taifa Jijini Dar es salaam 
yamekamilika,mara baada ya  hii leo viongozi wa vilabu hivyo ,Shilikisho la Soka nchiniTff , kampuni ya Selcom  kufanya kikao cha pamoja kujadili juu ya mapato yatakayopatikana kuhakikisha yanafika katika sehemu husika .
Kushoto  ni meneja miradi wa kampuni inayoshughulika na mfumo wa malipo ya kieletroniki ya Selcom Galus Lunyeta akiwa na Afisa habari wa Tff Afred Lucas hii Leo

Katika kikao hicho pia wamejadili juu ya viingilio ambapo  V.I.P ni shilingi 30,000 V.I.P B na C 20,000 Mzunguko 7,000,pia mashabiki wataweza kununua kadi kwa shilingi  7,000 tu hiyo hiyo  badala ya kutoa shilingi 3,000 ya gharama ya kadi peke yake ili kuweza kuondoa msongamano kwa mara ya kwanza.

Kuelekea katika mchezo huo Barabara ya chang’ombe itafungwa lakini  kutakuwa na wakala wa kuuza kadi ili kuondoa msongamano,Barabara  nyingine itakayofungwa ni ya Sigara.

Kadi zitakavyopatikana  katika Vituo vya mafuta vya TOTAL,PUMA na matawi yote ya Samaki Samaki, na kwa wakala mbalimbali kama Buguruni sheri,Ilala,Sinza,Mlimani City Uwanja wa Taifa N.K,pia imesisitizwa watu wapate Tiketi mapema ili kuondoa msongamano.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments