Majuma mawili baada ya Mwenyekiti wa Young Africans, Yusuph Manji kutangaza kuwavua uanachama baadhi ya wajumbe wa
kamati ya utendaji ya klabu hiyo kwa idhini ya wanachama waliohudhuria mkutano mkuu wa dharura uliofanyika jijini Dar es salaam, viongozi ha walivuliwa uanachama wamepeleka barua ya kupinga kuvuliwa uanachama katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Wajumbe wa kamati ya utendaji ya Young Africans ambao walivuliwa uanachama kwa baraka za mkutano mkuu wa dharura ul;iofanyika majuma mawili yaliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam,
wamewasilisha malalamiko yao katika ofisi za shirikisho la soka nchini TFF.
Katika mkutano huo uliazimia kuwafukuza uanachama, wanachama watatu wa klabu hiyo,ambao pia ni wajumbw wa kamati ya utendani ambao ni Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashim Abdallah walifukuzwa.
Afisa habari wa TFF Alfresd Lucas amethibitisha kupokelewa kwa malalamiko hayo, alipozungumza na waandishi wa habari hii leo ambapo amesema dhumuni kubwa la wajumbe hao kufanya hivyo ni kusaka haki yao ya kikatiba ambayo wanaamini ilikiukwa.

0 Comments