Ticker

6/recent/ticker-posts

ANGALIA REKODI/TAKWIMU YANGA SC vs AZAM FC LEO UWANJA WA TAIFA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 17,2016 SAA 06:34 MCHANA

Katika mchezo wa Ngao ya Jamii hii Leo unaoshiria kufunguliwa kwa pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL) 2016/17,kutakutanisha wababe wawili ambao ni Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC,mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga Sc na mchezo  huo utapigwa hii  leo saa 10.30 jioni.
Azam FC inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na makocha wapya kutoka Hispania, wakiongozwa na Kocha Mkuu Zeben Hernandez.

Ukiachilia mbali ujio wa makocha wapya, pia kuna baadhi ya sura kwa upande wa wachezaji, Azam FC ikiwasajili Wazimbabwe Bruce Kangwa, Francisco Zekumbawire, Muivory Coast Gonazo Bi Thomas, Waghana Enock Atta Agyei na beki kisiki Daniel Amoah.

Rekodi/Takwimu

Hii ni mara ya nne timu hizo kukutana kwa mwaka huu, ambapo Januari walikutana kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi na kuisha kwa sare ya bao 1-1, mtanange huo ulifuatiwa na ule wa mzunguko wa wa pili wa ligi ambao uliisha kwa sare nyingine ya 2-2 kabla ya Yanga kushinda 3-1 katika fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup).

Katika hatua nyingine, hii ni mara ya nne mfululizo kwa timu hizo kukutana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, Yanga ikifanikiwa kuibuka na ushindi mara zote.
Walianza kukutana mwaka 2013, Yanga wakishinda bao 1-0, lililofungwa na Salum Telela, ikashinda tena 3-0 (2014) kabla ya mwaka jana kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 8-7 kufuatia sare ya 0-0 baada ya dakika 90 za muda wa kawaida kumalizika.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)



Post a Comment

0 Comments