Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:MASHABIKI YANGA WAMLILIA MANJI,WAMTAKA AKILIMALI AJIONDOE KATIKA KLABU HIYO

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 16,2016 SAA 01:56 USIKU
Siku moja baada ya kuibuka kwa tetesi za kujiuzulu kwa mwenyekiti wa Young Africans Yusuf Mehboob Manji, hii leo
baadhi ya wanachama wa klabu hiyo walijikusanya katika makao makuu ya klabu hiyo yaliopo kwenye makutano ya mitaa ya Twiga na Jwangwani jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wanachama hao walionesha kuchukizwa na tetesi za kujiuzulu kwa mwenyekiti wao huku wakimtuhumu katibu wa baraza la wazee wa klabu ya Young Africans Ibrahim Yahya Akilimali ambaye anadiwa kutoa maneno mazito kwa Yusuf Manji kufuatia sakata la ombi lake la kutaka akodishwe timu pamoja na nembo ya klabu hiyo.

Wakati baadhi ya wanachama wa Young Africans wakiwa nje ya makao makuu ya klabu hiyo, wakuu wa matawi walifanya mkutano wao katika chumba cha mikutano klabuni hapo na kutoka na azimio la kulaani kauli zilizotolewa na Ibrahim Yahya Akilimali hadi kufikia hatua ya kumuudhi Manji na kusababisha fununu za kujiuzulu kwake.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa matawi mara baada ya kikao maalum kilichofanyika mapema hii leo, Robert Lyungu kasera ambaye pia ni mwenyekiti wa matawi ya wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni ameainisha maazimio waliyoyaafiki kwa pamoja.

SIKILIZA HAPA

Wakati wakuu wa matawi wakipitia maazimio hayo ambayo yatapelekwa kwenye kikao cha kamati ya utendaji, wanachama waliokua wamekusanyika nje ya makao makuu ya klabu ya Young Africans nao walipata nafazi ya kuzungumza .

Wanachama hao ambao walikua  jazba zao nao walizungumza huku wakimsihi Yusuf Manji abadilishe msimamo wake wa kutaka kujiuzulu nafasi yake ya uenyeketi.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments