Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:JOHN BOCCO AZUNGUMZA MECHI YAO AZAM FC NA YANGA

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 16,2016 SAA 01:15 JIONI
Mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Magwiji wa soka nchini Young Africans na Azam FC na  unayotarajiwa kuchezwa kesho katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam unatarajiwa kunufaisha wanafunzi wa shule ambao watapata mgao wa madawati kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jacob Ndugai

 Shirikisho la soka nchini TFF limesema kuwa sehemu ya fedha itakayopatikana kwa ajili ya viingilio zitatumika kuchangia kampeni ya madawati ambayo ilianzishwa na rasi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Kwa upande wa Azam FC wamesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho baada ya kikosi chao kuwa katika maandalizi chini ya kocha kutoka nchini Hispania tangu mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Rafael Bocco amesema wapo tayari kwa mchezo huo na wanaamini ushindani utakuwa wa hali ya juu hasa ukizingatia Young Africans wamekua na matokeo mazuri kwa mwaka jana wanapokutana.

MSIKILIZE JOHN BOCCO




 

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments