Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 19,2016 SAA 10:21 JIONI
Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17 inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi Agosti
20, 2016 kwa
michezo mitano huku Bingwa Mtetezi wa Kombe hilo 2015/16, Young
Africans ya Dar es Salaam ikisubiri hadi Agosti 31, 2016 kuanza kutetea taji
lake.
Young Africans
inatarajiwa kusafiri kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kucheza na
TP Mazembe kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kufanyika Agosti
23, mwaka huu.
Michezo itakayochezwa
kesho ni pamoja na Simba SC itakayoikaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja
wa Taifa, ulioko Chang’ombe Dar es Salaam, katika mchezo utakaoanza saa 10.00
jioni wakati Azam itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Azam FC
ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji.
Kadhalika
Stand United ya Shinyanga itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja
wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga sawa na Mtibwa Sugar itakayoikaribisha Ruvu
Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Manungu uliuoko Turiani, Mvomero mkoani
Morogoro wakati Prisons ya Mbeya itasafiri hadi Uwanja wa Majimaji ya Songea
kucheza na Majimaji FC ya huko.
Wakati ligi
ikianza, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaonya timu kuchezesha
wachezaji wa kigeni kama hawana vibali vya kuishi, kufanya kazi na leseni
inayomruhusu kucheza ligi husika kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni za Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Vibali vya
kuishi na kufanya kazi vinatolewa na Idara ya Uhamiaji Tanzania (Uhamiaji)
wakati leseni ya kucheza inatolewa na TFF. Vilevile tumeziagiza klabu kulipia
ada za ushiriki kwa kila timu; leseni za wachezaji, ada za wachezaji na ada za
mikataba. Mchezaji hatapewa leseni ya kucheza kama uongozi wa timu hautakamilisha
taratibu za malipo.
TFF linapenda
kuzikumbusha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwamba hatutatoa
leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati wa maombi ya
usajili, hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 68 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Kuu
ya Tanzania toleo la 2016/2017.
Kila timu
inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba,
sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba
hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa
TFF. Ni matarajio yetu kuwa kila klabu itatimiza wajibu wake ili kuondoa
migogoro kati ya timu na mchezaji na mchezaji na timu. Tunategemea kupata ushirikiano.

0 Comments