Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 19,2016 SAA 11:41 JIONI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Klabu
ya Majimaji ya
Songea, mkoani Ruvuma, Humphrey Millanzi kutokana na kifo cha mchezaji
wa zamani wa timu hiyo, Kelvin Haule kilichotokea jana Agosti 18, 2016
kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
Rais Malinzi amesema, amepokea taarifa za kifo cha Haule kwa masikitiko makubwa.
Rais Malinzi amemuelezea Haule kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika
mafanikio ya timku ya Majimaji ya Songea na Lipuli ya Iringa hivyo
ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha
kazi zake katika timu ambazo alichezea.
Salamu za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia zimekwenda kwa
familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo
wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa Kelvin Haule.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Kelvin Haule mahala pema peponi.
Bwana alitoa, Bwana alitoa, jina la Bwana lihimidiwe.
0 Comments