Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 19,2016 SAA 11:41 JIONI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kiingilio cha
Sh 2,000 kwa mzunguko na Sh 5,000 kwa jukwaa kuu wakati
timu ya taifa
ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 itakapocheza na
Amajimbos ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Madagascar,
mwakani.
Mchezo huo utaoanza saa 9.00 alasiri Jumapili Agosti 21, 2016 kwenye
Uwanja wa Azam ulioko Chamazi – Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam utachezeshwa na Mwamuzi Noiret Jim Bacari wa Comoro akisaidiwa na
Mmadi Faissoil na Said Omar Chebli wakati mezani atakuwa Ali Mohamed
Adelaid huku Kamishna wa mchezo huo atatoka Somalia ambaye anaitwa Amir
Abdi Hassan.
Jumamosi Agosti 6, 2016, Serengeti ilitoka sare ya 1-1 na Afrika
Kusini katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto,
Mji ulioko Kusini – Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote
yalipatikana kipindi cha pili yakiwa ni ya penalti kwa kila upande.
Afrika Kusini ndio walioanza kupata penalti katika dakika 65 iliyofungwa
na Luke Gareth kabla ya Ally Msengi kuisawazishia Serengeti Boys katika
dakika ya 70.
Penalti ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti
Boys kumfanyia madhambi Linamandla Mchilizeli wa Amajimbos ndani ya eneo
la hatari wakati ile ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa
Amajimbos kunawa mpira eneo la hatari. Mwamuzi wa mchezo huo alikuwa,
William Koto kutoka Lesotho.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi
amesema: “Watanzania wakaribie Chamazi, waje kutushangilia ili
tushangilie ushindi kwa pamoja kikosi change kiko vema na ninamshukuru
Mungu kwa hilo, akili yangu na akili za wachezaji wangu ni kumuondoa
Msauzi (Afrika Kusini).”
0 Comments