Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:KESSY AIDHINISHWA KUCHEZA YOUNG AFRICANS,SIMBA WATOA NENO

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 19,2016 SAA 12:53 JIONI 
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya mwenyekiti wake, wakili Richard
Sinamtwa imeliidhinisha jina la mchezaji Hassan Kessy kuichezea Young Africans huku akitakiwa kuilipa klabu yake ya zamani, Simba SC kwa kuvunja Mkataba.

Kessy anatakiwa kuilipa Simba SC Sh. Milioni 120 ili aanze kuichezea timu yake mpya ya Young Africans katika mashindano kuanzia sasa.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa katika mkataba wake na Simba, wote klabu na mchezaji walikubaliana atakayeuvunja atalipa dola za Kimarekani 60,000 zaidi ya Sh. Milioni 120,000 za Tanzania.

Kufuatia salata hilo afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Alfred Lucas amesema kamati ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji imeshatoa ruhusa kwa Kessy kuitumikia Young Africans, na masuala mengine yatachukua mkondo wake.


Hata hivyo uongozi wa klabu ya Simba umeyapokea maamuzi hayo ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kwa mtazamo wa shirikisho la soka nchini TFF kuendeleza kasumba ya kuibeba young Africans kwa makusudi ya watu wachache pasina kufuata taratibu na kanuni za kimkataba ambao ulikiukwa na Hassan Kessy.

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema uongozi wa Simba walitarajia maamuzi kama hayo yangetokea kutokana na utaratibu uliowekwa ndani ya shirikisho hilo kwa kumbukumbu za malalamiko ambayo waliwahi kuyawakilisha kwao lakini yalishindwa kufanyiwa kazi kwa wakati.

MSIKILIZE HAJI MANARA AKIZUNGUMZA  HAPA

K

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments