Meneja mpya wa kikosi cha Simba Mussa Hassan Mgosi ameweka
wazi mustakabali wa kazi zake ndani ya klabu hiyo ambayo
ameitumikia kwa
vipindi viwili tofauti kabl ya kuamua kustaafu mwishoni mwa juma lililopita.
Mgosi ambaye alitimkia Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
katika klabu ya Daren Motema Pembe na kasha kurejea nchini na kuzitumikia JKT
Ruvu kabla ya kwenda Mtibwa Sugar na hatimae kurejea Msimbazi, amesema dhamira
yake kubwa ni kuhakikisha heshima wa Simba inarejea kwa kuwahamasisha wachezaji
waliosajiliwa kwa ajili ya msimu wa 2016/17.
Amesema kiu yake kubwa ni kutaka kuona heshima na mafanikio
ya Simba anaruzi kama ilivyokua miaka ya nyuma kabl ya kuanza kusota katika
nafasi ya tatu hadi ya nne katika msimamo wa ligi kuu tangu mwaka 2011.
SIKILIZA HAPA
0 Comments