Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ulikuwa unaashiria kufunguliwa kwa pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) 2016/17,ambapo wababe hao wawili bingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC,na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga Sc walitoka sare ya kufungana maba 2 - 2 katika dakika 90 za kawaida
Mmoja wa wafungaji katika mcezo huo ni Shomari Kapombe, ambaye yeye amezungumza na Jamii na Michezo na kutoa shukurani kwa waliomuombe wakati akiwa majeruhi na amewaahidi mambo makubwa zaidi ya msimu uliopita huku akitolea mfano wa juhudu zake katika mchezo wa jana ambazo ziliwarejeza Azam FC katika mchezo.
SIKILIZA HAPA
Katika Penalti upande wa Azam fc wote walipata ambao ni John Raphael Bocco,Nahodha Msaidizi Himid Mao Mkami, Shomary Kapombe pamoja na Kipre Michael Balou.
Upande wa Yanga Kipa Deo Munishi ‘Dida’ ndiye pekee aliyefunga penalti,huku mkwaju wa mchezeji mpya wa klabu hiyo Hassan Ramadhani Kessy ukipanguliwa na kipa wa Azam Fc Aishi Salum Manula,na penalti ya kiungo wa Rwanda, Haruna Fadhil Niyonzima alipaa juu ya lango.


0 Comments