Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA YAZINDUA UJENZI WA UWANJA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 19,2016 SAA 01:19 USIKU
Ramani ya Uwanja wa Simba Utakavyokuwa
Rais klabu ya Simba Evans Elieza Aveva hii leo amezindua Ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Bunju kwa kuwashirikisha wanachama na
mashabiki wa klabu hiyo ambao walifurika katika eneo la uwanja huo lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Aveva amezindua Ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Bunju kwa kuwataka wanachama na mashabiki wa klabu ya nchini kote, kujitoa kwa hali na mali ili kufanikisha azma waliyoikusudia.

Amesema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kutaka kukiwezesha kikosi cha Simba kuwa na mahala maalum pa kufanyia mazoezi yake, tofauti na hivi sasa ambapo kimekua kikifanya maandalizi katika viwanja vya kukodi.

Naye mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAG ambayo inashirikina na klabu ya Simba katika masuala ya kimaendeleo Imani Kajula alipata nafasi ya kuzungumza na wanachama waliokua wamehudhuria uwanjani hapo na kueleza mikakati ya kufanikisha Ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Bunju.


Kajula pia alifanya mnada wa jezi za wachezaji wane wa samba, Laudit Mavugo, Mohamed Hussein Tshabalala, Jonas Mkude pamoja na Shiza Kichuya ambazo zote kwa pamoja zilinunuliwa na wanachama tofauti wa Simba na kufanikisha upatikanaji wa shilingi miliini 14 ambazo zitaingizwa katika Ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Bunju.

Baada ya zoezi hilo, wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba walianza kujitokeza mmoja baada ya mwingine na kutoa michango yao ya pesa na wengine wakiahidi kutoa saruji pamoja na matofali.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments