Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 6,2016 SAA 03:10 USIKU
| Ibrahim Abdallah wa Serengeti Boys akibanwa na Beki wa Amajimbos, Sechala Makoena |
Ikicheza mbele
ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Naibu
Balozi wa Tanzania
nchini Afrika Kusini, Rosemary Chambe Jairo, timu ya soka ya
vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys leo imegoma
kupoteza mchezo dhidi ya wenyeji Afrika Kusini baada ya kuibana Amajimbos na
kutoka sare bya bao 1-1.
Katika mchezo
huo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko Kusini
–Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote yalipatikana kipindi cha pili
yakiwa ni ya penalti kwa kila upande. Afrika Kusini walianza kupata penalti katika
dakika 65 iliyofungwa na Linamandlia Mchilizeli kabla ya Ally Msingi
kuisawazishia Serengeti Boys katika dakika ya 70.
Penalti ya Afrika
Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti Boys kumfanyia madhambi Mchilizeli wa Amajimbos ndani ya eneo la hatari wakati
ile ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa Amajimbos kunawa mpira
eneo la hatari.
Afrika Kusini
iliyoanza kwa kasi dakika 10 za mwanzo wa mchezo huo, ilipotea dakika zote 30
za kipindi cha kwanza ambao kukosa bahati na umakini kidogo tu kwa nyota wa
Serengeti Boys kulisababisha kukosa mabao matano yakiwamo mawili yaliyogonga
mwamba hivyo kuwatia hasira Serengeti Boys ambao walionyesha kuwa na njaa ya
mabao.
| Naibu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Rosemary Jairo (wa pili kushoto) na Rais wa TFF, Jamal Malinzi wakiwa wamezungukwa na nyota wa Serengeti Boys |
Kubanwa katika
kipindi cha kwanza, kulisababisha Kocha Mkuu wa Amajimbos kufanya mabadiliko ya
wachezaji wote watatu kipindi cha pili, wakati Bakari Shime kwa upande wake
alimpumzisha Ibrahim na nafasi yake kuchukuliwa na Muhsin ambaye alisaidia kuendedlea
kuwabana Afrika Kusini waliokjuwa wanawategemea nyota kama na Mswati Mavuso na
Lethabo Mazibuko.
Shukrani za
pekee zinaweza kwenda kwa Kipa Ramadhani Kabwili aliyeokoa hatari nyingi
ikiwamo mpira uliokuwa unakwenda golini uliotokana na adhabu ndogo. Kadhalika Msengi
aliyekuwa nyota wa mchezo huo akimiliki vema idarta ya ulinzi akishirikiaana
nDickson Job.
Shime maarufu
kama Mchawi Mweusi alisema: “Nashukuru kwa matokeo haya. Si mabaya kwangu. Tunarudi
nyumbani kujipanga. Afrika Kusini ilikuwa inanitia hofu ndio maana nilisema
mechi itakuwa ngumu.”
Kwa upande
wake, Naibu Balozi Rosemary alisema: “Ahsanteni vijana (Serengeti Boys) kwa
kulinda heshima yangu,” wakati Malinzi alisema: “Sina mengi. Mkiwafunga Afrika
Kusini Agosti 21, 2016 kambi inapigwa tena nje ya nchi. Sijui ni nchi gani,
lakini mtakwenda kujiandaa nje ya nchi.”
Katika mchezo
huo, Kikosi cha Serengeti kilikuwa: Ramadhani Kbawili, Israel Mwenda, Nickson
Kibabage, Ally Msengi, Dickson Job, Shaban Ada, Kelvin Naftal, Ally Ng’anzi, Ibrahim
Abdallah/Muhsin Makame (Dakika ya 72), Asad Juma na Mohammed Rashid.
Afrika Kusini:
Glen Tumelo, Mswati Mavuso, Luke Donn, Sechaba Makoena, Kwenzokuhle Shinga,
Mjabulise Mkhize, Bonga Dladla, Linamandla Mchilizeli, Luke Gareth, James Monyane
na Siphamandla Ntuli.
0 Comments