Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:ANGALIA SIMBA DAY ILIVYOKUWA LEO,MNYAMA AMUANGAMIZA LEOPARDS 4 -0

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 8,2016 SAA 02:10 USIKU
Klabu ya Simba hii Leo 8 Aug,2016 imeazimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake kwa kuifunga timu ya AFC Leopards mabao 4 -0
katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Simba ambao walianza na mchakato walioupa jina la Simba wiki,walianza kwa Azimio la kufanya usafi siku ya jumamosi ambapo ni sehemu ya kukamilisha shughuli za Simba wiki ambazo zilitangazwa na uongozi wa klabu hiyo kupitai raisi wake Evance Aveva.

Kikosi cha Simba Leo
kikosi Cha AFC Leopards leo
Mabao ya Simba katika mchezo huo wa Simba Day yalifungwa na Ibrahim Ajibu ambaye alifunga mabao mawili,dakika ya 38 na kipindi cha pili dakika ya 11.
Kipindi cha pili Katika dakika ya 21 mchezaji mpya Shiza Kichuya alipachika bao la 3 la Simba na Bao la 4 lilifungwa na mchezaji mpya pia  Laudet Mavugo Dakika ya 36 ya kipindi hiko cha pili.
 ANGALIA PICHA













KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments