Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:ANGALIA SIMBA SC WALIVYOPIGA USAFI LEO

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 6,2016 SAA 01:03 USIKU

Uongozi, wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba hii leo wamefanya usafi katika mtaa wa Msimbazi maeneo yanayozunguuko
majengo ya klabu hiyo kongwe ambayo mwanzoni mwa juma lijalo itakua na inaazimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.

Azimio hilo la kufanya usafi ni sehemu ya kukamilisha shughuli za samba wiki ambazo zilitangazwa na uongozi wa klabu ya Simba kupitai raisi wake Evance Aveva majuma mawili yaliyopita mbele ya waandishi wa habari.

Makamu wa rais wa klabu ya Simba Geoffrey Nyange  Kaburu alishiriki katika zoezi hilo ambalo lilichukua zaidi ya saa moja, na mara baada ya kukamilishwa kwake, aliwashukuru wanachama pamoja na mashabiki waliojitokeza.

Naye mbunge wa jimbo la Ilala ambapo ndipo klabu ya Simba ilipo, Mussa Azzan Zungu  alishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika mtaa wa Msimbazi na alipata nafasi ya kuzungumza na wanachama pamoja na mashabiki walioshiriki katika zoezi hilo.

Zungu alitoa shukurani pamoja na kuwataka viongozi wa klabu ya Simba kuwa kitu kimoja ili kuhakikisha klabu hiyo inapiga hatua na kuondoka hapa ilipo sasa.

ANGALIA PICHA







KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)


Post a Comment

0 Comments