Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 5,2016 SAA 12:53 JIONI
Hatimae uongozi wa klabu ya Young Africans, umetangaza
ajenda za mkutano mkuu wa wanachama uliopangwa kufanyika kesho katika
ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Young Africans ilitoa taarifa ya kuitishwa kwa mkutano huo
mkuu mwanzoni mwa juma hili pasina kuwa na agenda ambazo zitajadiliwa halia
mbayo ilizua tafrani miongoni mwa wanachama na kufikia hatua kwa baadhi yao
kuuita mkutano huo ni batili.
Meneja wa masoko na uratibu wa matawi na wanachama wa Young
Africans, Omar Kaya alibeba jukumu la kuzitaja agenda za mkutano mkuu wa
wanachama ambao umepangwa kuanza mishale ya saa tatu asubuhi.
Hata hivyo suala la kubadilishwa kwa mfumo uendeshwaji nalo
limezungumza na Meneja wa masoko na uratibu wa matawi na wanachama wa Young
Africans, Omar Kaya baada ya kuibuka kwa tetesi kutoka kwa baadhi ya wanachama
ambao walionyesha kupotezwa na maazimio yaliyofikiwa na wapinzani wao Wekundu
wa msimbazi Simba mwishoni mwa juma lililopita.
SIKILIZA HAPA
Wakati huo huo Young Africans wameohoji zoezi la kukabidhi
vifaa ambalo lilifanywa jana na wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara,
kampuni ya mawasilino ya Vodacom kufuatia nembo ya kampuni ya vifaa hivyo
kutokua na maslahi na klabu yao pamoja na klabu nyingine zitakazoshiriki ligi hiyo.
Omar Kaya amesema kuna haja kwa TFF kupitia bodi ya ligi
wakalitolea ufafanuzi suala hilo ambalo linaonekana kumnufaisha zaidi mdhamini
wa ligi kuu pamoja na kampuni inayoonekana katika vifaa vilivyotolewa hapo jana


0 Comments