Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 6,2016 SAA 01:30 USIKU
| Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji akizungumza hii leo |
Historia imeandikwa kwa klabu ya Yanga siku ya Leo 6 Aug.2016 katika Mkutano Mkuu wa dharula uliofanyika leo ukumbi wa
Diamond jubilee, Dar es Salaam baada ya Wanachama hiyo ambayo ni mabingwa wa Tanzania bara kukubali kumkodisha klabu hiyo Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kwa miaka 10 .
Katika mkutano huo Manji ameomba apewe klabu hiyo kwa miaka 10 na katika kipindi
hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki
kwa wanachama.
| Wanachama wa Yanga wakifuatilia Mkutano |
mkutano huo umekubali kipindi hicho cha miaka 10, timu, nembo
ya klabu zote zitakuwa chini ya Manji.
Katika hatua nyingine mkutano huo umeazimia kuwafukuza
uanachama, wanachama watatu wa klabu hiyo, Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashim
Abdallah walifukuzwa.
Taarifa za mapungufu ya wajumbe wa kamati ya utendaji
pamoja na wanachama hao wa Young Africans ziliwasilishwa katika mkutano huo na kaimu mtendaji mkuu Baraka
Deusdetit.
| Kaimu mtendaji mkuu Baraka Deusdetit |
Mara baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo Manji aliwaambia
wanachama hayuko tayari kufanya kazi na Wajumbe hao wa Kamati ya Utendaji na
akaomba wanachama wanaowataka wajitokeze kupiga kura, lakini hakuna aliyeinuka.
Baada ya kurudia kuita mara tatu, Hashim pekee kati ya
watatu hao ambaye alikuwepo mkutanoni ukumbi wa Diamond Jubilee, akainuka na
kuondoka.
Mwanachama mwingine, Siza Lyimo ambaye Manji alitaka
aondoke, yeye aliomba msamaha na wanachama wakamsamehe na Mwenyekiti huyo
akabariki msamaha huo.
Mkemi na Nyenzi hawakutokea kwenye Mkutano huo.

0 Comments