Ticker

6/recent/ticker-posts

MARIO BAROTELLI AMEKUTANA NA MOURINHO WA MANCHESTER UNITED, NA HIKI NDICHO ALICHOKIFUATA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 17,2016 SAA 08:59 MCHANA
Mshambuliaji wa LIVERPOOL Mario Balotelli ameripotiwa kufanya mazungumzo na Kocha wa Manchester United Jose
Mourinho.

Mshambuliaji huyo wa Italia alikuwa akiitajika kwa ziada katika uwanja wa Anfield na kocha
Jurgen Klopp amemwambia atafute klabu mpya .

Imedaiwa Balotelli ametafuta ushauri kwa kocha wa Manchester United, ambaye aliweza kuwa naye katika klabu ya Inter Milan.

Mourinho imefahamika kuwa amemwambia mshambuliaji huyo mtukutu kubadili mtazamo wake na kupunguza madai yake  ya mshahara.

Balotelli anasimamiwa na wakala mkubwa Mino Raiola na ripoti zisema kuwa sasa anamsaidia kufanya kazi ya kuondoka Merseyside baada ya uhamisho wa Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan. 


KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments