Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 17,2016 SAA 01:49 USIKU
Azam fc ndiyo mabingwa wapya wa Ngao ya Jamii baada ya hii Leo kufanikiwa kuibuka na ushindi wa penalti 4 kwa 1.
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam unaoashiria kufunguliwa kwa pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara (VPL)
2016/17,ambapo wababe hao wawili bingwa wa Afrika
Mashariki na Kati Azam FC,na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga Sc walitoka sare ya kufungana maba 2 - 2 katika dakika 90 za kawaida
Hii ni mara ya nne mfululizo kwa timu hizo
kukutana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, Yanga ikifanikiwa kuibuka na
ushindi mara tatu.
Walianza kukutana mwaka 2013, Yanga wakishinda bao 1-0, lililofungwa
na Salum Telela, ikashinda tena 3-0 (2014) na mwaka (2015 ) jana Yanga kushinda
kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 8-7 kufuatia sare ya 0-0 baada ya
dakika 90 za muda wa kawaida kumalizika.
Katika mchezo wa leo Mabao yote ya Yanga yakifungwa Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma moja kwa Penalti dakika ya 20 na lingine dakika 2 baadaye yaani dakika ya 22, na Azam FC mabao yao yalifungwa na beki Shomary Salum Kapombe dakika ya 74 pamoja na Nahodha John Raphael Bocco dakika 90'.
Katika mchezo wa leo Mabao yote ya Yanga yakifungwa Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma moja kwa Penalti dakika ya 20 na lingine dakika 2 baadaye yaani dakika ya 22, na Azam FC mabao yao yalifungwa na beki Shomary Salum Kapombe dakika ya 74 pamoja na Nahodha John Raphael Bocco dakika 90'.
Katika Penalti upande wa Azam fc wote walipata ambao ni John Raphael Bocco,Nahodha Msaidizi Himid Mao Mkami, Shomary Kapombe pamoja na Kipre Michael Balou.
Upande wa Yanga Kipa Deo Munishi ‘Dida’ ndiye pekee aliyefunga penalti,huku mkwaju wa mchezeji mpya wa klabu hiyo Hassan Ramadhani Kessy ukipanguliwa na kipa wa Azam Fc Aishi Salum Manula,na penalti ya kiungo wa Rwanda, Haruna Fadhil Niyonzima alipaa juu ya lango.
ANGALIA PICHA





0 Comments