Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY 15,2016 SAA 04:14 USIKU
Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania, imeandaa kozi mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kwa waamuzi
katika michuano ya kimataifa sambamba na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la
Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017.
Kozi hiyo MA (Members Associations) itaanza kwa
waamuzi wenye Beji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA)
ambao kwa sasa wako 18 hapa Tanzania na wengine 12 wa ‘Elite’ ikiwa na
maana ya waamuzi wanaotarajiwa kuveshwa Beji za FIFA. Darasa la waamuzi
hao litakuwa na waamuzi 30.
Waamuzi hao wenye Beji ya FIFA na wale
wanaotarajiwa kuveshwa beji hiyo, wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam
Julai 23, 2016 ambako kwa mujibu wa ratiba wataanza program ya kozi hiyo
kwa kupima kasi ya kukimbia siku inayofuata Julai 24, 2016 wakisimamiwa
na wakufunzi kutoka FIFA.
Mara baada ya programu hiyo, kozi itaendelea kwa
waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la
Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) na makamishna wa
michezo kwa msimu wa 2016/2017 na kwamba wahusika wote watajigharamia
gharama zote.
Waamuzi hao wa ligi ya ndani wataripoti na
kujisajili Kituo cha Dar es Salaam Julai 29 na siku inayofuata Julai 30,
2016 na Julai 31, 2016 watakuwa na kozi ya kitathmini kasi kwa kukimbia
kabla ya Agosti 1 na 2, 2016 kuwa na semina darasani na mitihani wakati
Agosti 3, 2016 kutakuwa na semina na mitihani kwa makamishna mbalimbali
wa michezo ya mpira wa miguu.
0 Comments