Klabu ya Yanga kutoka jijini Dar es salaam hii leo imeshindwa kutamba kwa mara nyingine tena kwenye uwanja wa nyumbani
baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Medeama SC ya Ghana katika mchezo wa Kundi A michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Matokeo hayo sasa yanaifanya Yanga ipate pointi 1 na ni ya mwisho katika kundi lake, baada ya awali kufungwa 1-0 na MO Bejaia nchini Algeria na TP Mazembe ya DRC 1 -0 jijini Dar es Salaam pia.Medeama inabaki nafasi ya tatu kwa pointi mbili, nyuma ya MO Bejaia yenye pointi nne na TP Mazembe pointi sita.
Mchezo huo uliochezeshwa na refa Ibrahim Nour El Din, aliyesaidiwa na washika vibendera Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wote wa Misri,mabao yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza.
Saimon Msuva akimtoka mchezaji wa Medeama SC ya Ghana |
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao lilifungwa na mshambuliaji wao Donald Dombo Ngoma dakika ya pili tu ya mchezo |
Bao la Yanga lilifungwa na mshambuliaji wao Donald Dombo Ngoma dakika ya pili tu ya mchezo, akimalizia pasi ya Mzimbabwe mwenzake, Thabani Kamusoko na kumchambua kipa Daniel Adjei.
Bao la Medeama lilifungwa Dakika ya 17 na mfungaji Bernard Donso akimalizia kona ya Enock Atta Adjei.
0 Comments