Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY 21,2016 SAA 11:00 JIONI
Shirikisho la soka
nchini Tanzania TFF limeburuzwa mahakamani na kampuni ya Smart Sports kwa madai
ya kutoa hundi hewa kwa
kampuni hiyo.
kampuni hiyo.
Kampuni ya Smart Sports
imeishtakia TFF kwenye mahakama ya kisutu ikataka ilipwe Shilingi milioni 15
baada ya kuiuzia TFF vifaa vya mazoezi kwa timu za Taifa.
Katika mahakama ya
hakimu mkazi Kisutu, kesi ya hundi hewa inayolikabili shirikisho la soka Nchini
imeanza kusikilizwa Alhamisi hii.
Kesi hiyo namba 175 ya
2016 imefunguliwa June 27 mwaka huu, ambapo Smart Sports imeilalamikia TFF kwa
kuwapa hundi hewa.
Mwaka 2014 Smart Sports
iliuzia TFF vifaa vya michezo pamoja na kutoa huduma ya usafiri kwa timu za
Taifa, zenye thamani ya shilingi milioni 31.
February 23 TFF ikamkabidhi hundi Mkurugenzi
wa Smart Sports Bwana GEORGE Wakuganda, lakini hundi hiyo ikashindikana kufanya
malipo yaani imebaounce.
March 29 TFF ikakabidhi tena hundi kwa
Wakuganda, na baada ya kwenda banki akakutana na hali ile ile.
Hapo ndipo Wakuganda akaanza harataki za kudai
haki yake mahakamani.
March 29 Smart Sports ikawaandikia barua TFF
kuulizia malipo hayo lakini TFF haikujibiwa.
June 15 2016 Smart Sports kupitia wakili wake
akaindia barua TFF
lakini TFF ikauchuna
tena.
Kesi hiyo imesikilizwa Alhamisi hii kwa mara
ya kwanza lakini TFF hawakutokea mahakamani licha kupekelekewa barua ya wito
iliyowafikia June 11 mwaka huu.
Nae mkurugenzi wa Smartsports amesema amemua
kwenda mahakamani baaada ya kuona TFF hawataki kulipa deni kiungwana.
Kesi hiyo itasikilizwa
tean August 3 mwaka huu.
0 Comments