Kozi za Waamuzi wa Mpira wa Miguu wa Tanzania
sasa itaanza Julai 25, 2016 badala ya Julai 24, 2016 kama ilivyotangazwa
hapo
awali.
Kozi hiyo itaanza moja kwa moja kwa waamuzi wenye
Beji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) ambao kwa sasa
idadi yao ni 18 na waaamuzi waandamizi ambao idadi yao ni 12.
Itaanza kwa ratiba ya waamuzi wote kuchukuliwa
vipimo (physical fitness test) kwa kila mwamuzi chini ya wawezeshaji wa
kozi hiyo kutoka FIFA.
Wawezeshaji hao ni Carlos Henrique kutoka Afrika
Kusini, Mark Mzengo kutoka Malawi na Felix Tangawarima wa Zimbabwe.
Waamuzi hao wenye Beji ya FIFA na wale wanaotarajiwa kuveshwa beji hiyo,
wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam Julai 24, 2016.
Baada ya vipimo, darasa la waamuzi hao litaanza
kwa nadharia na vitendo. Darasa hilo litafikia mwisho Julai 29, 2016
kabla ya kuanza darasa la waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili
(SDL) kwa msimu wa 2016/2017.
Mara baada ya programu hiyo, kozi itaendelea kwa
waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la
Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) na makamishna wa
michezo kwa msimu wa 2016/2017 na kwamba wahusika wote watajigharamia
gharama zote.
Waamuzi hao wa ligi ya ndani wataripoti na
kujisajili Kituo cha Dar es Salaam Julai 28, 2016 na na Julai 29, 2016
na Julai 30, watakuwa na kozi ya kitathmini kasi kwa kukimbia kabla ya
Agosti 1 na 2, 2016 kuwa na semina darasani na mitihani wakati Agosti 3,
2016 kutakuwa na semina na mitihani kwa makamishna mbalimbali wa
michezo ya mpira wa miguu.
0 Comments