Aliyekua kocha mkuu wa Azam FC Joseph Marius Omog, hii leo amatangazwa rasmi na uongozi wa klabu ya Simba kuwa mkuu wa
benchi la ufundi la klabu hiyo ambayo imekua ikikabiliwa na mtihani wa kushindwa kurejea katika kilele cha mafanikio kama ilivyokua miaka ya nyuma.
benchi la ufundi la klabu hiyo ambayo imekua ikikabiliwa na mtihani wa kushindwa kurejea katika kilele cha mafanikio kama ilivyokua miaka ya nyuma.
Shughuli ya kumtangaza Omog ilifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Regency jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa klabu ya Simba pamoja na waandishi wa habari.
Dhima ya kumtangaza Omog, ilibebwa na rais wa klabu ya Simba Evance Elieza Aveva ambapo alisema kuletwa kwa kocha huyo mwenye vigezo vya kukinoa kikosi cha Wekundu Wa Msimbazi ilikua ni moja ya mikakati yake iliyopewa Baraka na kamati ya utendaji klabuni hapo.
SIKILIZA HAPA
<Aveva amesema wana uhakika Omog ataweza kufikia lengo wanalolikusudia wao kama viongozi, pamoja na kumaliza tatizo la kusaka mafanikio ya kutwaa ubingwa kwa msimu ujao wa ligi.
<Aveva amesema wana uhakika Omog ataweza kufikia lengo wanalolikusudia wao kama viongozi, pamoja na kumaliza tatizo la kusaka mafanikio ya kutwaa ubingwa kwa msimu ujao wa ligi.
Mbali na kumtangaza Joseph Omog kama kocha mkuu wa klabu ya Simba, Evance Aveva akatumia nafasi ya kukutana na wanahabari hii leo kumtangaza katibu mkuu mtendaji mpya Patrick Kahemele ambaye ameanza rasmi kazi zake hii leo.
Baada ya utambulisho huo, kocha Omog alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo, na kueleza furaha na matarajio yake ya kiutendaji hasa katika kipindi hiki ambacho amekuja nchini kwa mara ya pili kwa kuitikia wito wa klabu ya Simba.
Omog Amesema anatambua changamoto zinazoikabili klabu ya Simba, hivyo hana budi kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha malengo yanayokusudiwa yanatimizwa kwa wakati muafaka.
Hata hivyo kocha huyo aliyeipa ubingwa wa Tanzania bara Azam FC mwaka 2014 amesisitiza suala la ushirikiano, ili kuyatimiza yote aliyoyakusudia kuyafanya akiwa na wekundu hao wa Msimbazi.
Wakati huo huo katibu mkuu mtendaji mpya wa klabu ya Simba, Patrick Kahemele naye akazungumza namna anatavyoanza kazi yake klabuni hapo huku akiainisha baadhi ya mambo ambayo yatakua ya msingi.
Amesema jukumu kubwa alilonalo ni kusaidia mafanikio yanapatikana kwa kuirejeshea Simba heshima yake ya kufanya vyema katika ligi kuu ya soka Tanzania pamoja, pamoja na kuwatumia vizuri wanachama wa klabu hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo.
0 Comments