Mkufunzi Jose Mourinho amesema kuwa yuko tayari kuchukua jukumu la kuifunza Manchester United, lakini
akaonekana pia kumkejeli meneja wa Arsenal Arsene Wenger.
akaonekana pia kumkejeli meneja wa Arsenal Arsene Wenger.
katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari Mourinho kaongea vitu vingi ikiwemo kutoa kauli zake ambazo zimetafsirika kama kejeli kwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwa kukosa Ubingwa kwa miaka mingi.
Amesema ''niko mahala nitakapo''.
Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 aliongezea: ''Nadhani ni kazi ambayo kila mtu anahitaji na sio wengi ambao huipata na mimi nimeipata''.
Alipoulizwa iwapo ana chochote cha kujionyesha baada ya kufutwa kazi akiwa Chelsea, alijibu, akionekana kumrejelea Wenger: ''Kuna mameneja ambao hawajashinda mataji kwa kipindi cha miaka 10 iliopita. Wengine bado kabisa. Mara yangu ya mwisho kushinda taji ni mwaka uliopita''.
Mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea anachukua mahala pake Louis Van Gaal,ambaye alifutwa kazi baada ya United kushinda kombe la FA mnamo mwezi Mei.
Mourinho anasema kuwa anachukizwa kuona kwamba United haitashiriki katika mechi za kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao lakini akasisitiza kuwa yuko Old Trafford kushinda mataji.
Nataka kila kitu,alisema.Nataka kushinda mechi,nataka kucheza vizuri sitaki kufungwa magoli.nataka mashabiki kutuunga mkono.
''Ni kweli hatuwezi kupata kila kitu, lakini tunataka''.
“Hata hivyo siwezi kuficha kusikitishwa kwangu na Man United kukosekana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, naimani ni kwa msimu mmoja tu ndio tutakuwa hatushiriki michuano hiyo ila hadi July 2017 tutalazimika kuhakikisha tunashiriki michuano hiyo”
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
.
0 Comments