Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO/PICHA:JERRY MURO LEO AMEFIKA TFF,HIKI NDICHO ALICHOAMBIWA..sikiliza hapa...

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY 2,2016 SAA 11:37 JIONI

Kamati ya maadili ya shirikisho la soka nchini TFF, hii leo imekutana kwa ajili ya kusikiza mashauri matatu yaliyowasilishwa
mbele yao na katibu mkuu wa shirikisho hilo Celestin Mwesigwa.

Mashauri yaliyofikishwa mbele ya kamati hiyo yalikua dhidi ya afisa habari wa klabu bingwa Tanzania bara, Young Africans Jerry Muro, mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF kutoka mkoani Shinyanga Mbasha Matutu pamoja na katibu mkuu wa chama cha soka mkoa wa Mwanza MZFA, Nasoro Mabrouk.

Kamati hiyo ya maadili imesikiza mashauri yote na kubaini kulikua na kasoro kadhaa na hivyo wamemuagiza katibu mkuu wa TFF Celestin Mwesigwa kufanya utaratibu wa kuyawasilisha upya.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Wilson Ogunde amesema kuhusu mashauri ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF kutoka mkoani Shinyanga Mbasha Matutu pamoja na katibu mkuu wa chama cha soka mkoa wa Mwanza MZFA, Nasoro Mabrouk, wameagiza baadhi ya dosari kurekebishwa.

Kwa upande wa shauri la afisa habari wa Young Africans, Jerry Muro Ogunde amesema kamati yake imelipitia lakini walikutana na kikwazo cha muhusika kutofika mbele yao kwa ajili ya kujitetea, licha ya upande wa TFF kuthibitisha walimfikishia taarifa za kumtaka afike kwenye kikao.

SIKILIZA HAPA
OOgunde hakuishia hapo bali aliendelea kufafanua kwa kina namna kamati yake ilivyolifanyia kazi suala hilo a mbaloliliibua utata na kubaini kulikua na makosa ya wito uliotolewa na Jerry Muro kufika mbele yao, hivyo wameagiza taratibu mpya za kuitwa kwa afisa habari huyo wa Young Africans kufanywa tena.

Hata hivyo maamuzi hayo ya kamati ya maadili ya shirikisho la soka nchini TFF yamepokelewa kama ushindi kwa aliyekuwa mtuhumiwa Jerry Muro ambaye alizungumza na vyombo vya habari akiwa katika viunga vya shirikisho hilo.

Muro amesema anaamini maamuzi yaliyotangazwa na kamati ya maadili dhidi yake, ni sawa na ushindi mwingine kwa klabu yake, huku akitoa angalizo kwa katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa.


Kama hiyo haitoshi Jerry Muro akaendelea kusisitiza kwamba anaamini shauri hilo limeshamalizika na ametoa ushari wa kuacha soka la Tanzania kuingia katika hatua nyingine za kuendelezwa na kuachwa kwa mikakati ya malumbano.

ANGALIA PICHA









KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments