Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA JUU YA GARETH BALE KUVUNJA REKODI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 21,2016 SAA 11:07 JIONI
Katika michuano ya kombe la Euro inaweza kuwa habari njema kwa mashabiki wa Euro 2016 kuiona Urusi wenye
mashabiki wenye fujo ikitolewa katika mashindano hayo, baada ya kulazwa na Wales mabao matatu kwa nunge katika mechi ya mwisho na muhimu ya hatua ya makundi jana usiku.
Aaron Ramsey na Neil Taylor na Gareth Bale walifunga mabao hayo muhimu na kuisaidia timu hiyo ya kocha Chris Coleman ikiwa imejihakikishia nafasi katika mkumbo wa pili kwa mara ya pili katika historia yake.
Wapinzani wao wa jadi England walimudu sare tasa dhidi ya Slovakia mjini Saint-Etienne na kuhakikisha kuwa Wales wanafuzu kwa raundi ya pili ya mashindano hayo kama vinara wa kundi B.
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Wales sasa watachuana na mshindi wa tatu katika kundi C A ama D.
Wales na England zimefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Euro baada ya mechi zake za kundi B kukamilika.

GARETH BALE AVUNJA REKODI
13108612_1134282759961344_2144088758_n
Mchezaji wa Real Madrid, Galeth Bale amefanikiwa kuivunja rekodi ya Ivor Allchurch aliyoiweka miaka 58 kwenye timu ya taifa Wales baada ya kufunga kwenye mechi tatu mfululizo kwenye michuano ya kombe la Euro yanayoendelea huko Ufaransa na kufikisha magoli 23 katika mechi 59 alizocheza mpaka sasa.

Ivor Allchurch alifanikiwa kuifungia timu ya taifa jumla ya magoli 23 katika mechi 68 alizowahi kucheza na timu hiyo tangu alipoitwa kwa mara ya kwana mwake 1950 mpaka 1966 na kumfanya kuwa mfungaji wa muda wote kwenye hiyo timu ya taifa [Wales].
chemical-kama-ipo
Bale alifanikiwa kufunga goli lake la tatu kwenye mashindano hayo walipoifunga timu ya Urusi jumla ya magoli 3-0 kwenye mashindano hayo ya Euro huku akiwa tayari ameshazifunga timu za Slovakia na Uingereza walizokuwa nazo kwenye kundi moja la michuano hiyo.
Bale ameanza michuano ya Uero 2016 akiwa mwenye bahati kubwa ambayo haijawahi kuwatokea wachezsaji wengi tangu walipofanya hivyo kina Milan Baros wa Jamhuri ya Czech na Ruud van Nistelrooy wa Uholanzi waliofunga mechi zote tatu katika Euro 2004.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments