Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:MILLION 44 ZAIMARISHA UWANJA WA TAIFA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 17,2016 SAA 02:29 USIKU
Naibu waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Anastazia Wambura akipokea msaada wa mageti kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TING, Dk. Vernon Fernandes 
Naibu waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Anastazia Wambura hii leo amepokea msaada wa mageti yenye thamani ya Shilingi millioni 44 kutoka katika
kampuni ya TING kwa ajili ya kuwekwa katika vyoo vya uwanja wa taifa.

Wambura amesema mara baada ya kufanya ukaguzi katika uwanja huo aamegundua uhalibifu katika maeneo mbali mbali katika vyoo vya uwanja huo,ndio maana akaomba msaada kutoka kwa wadau ili kuweza kusaidia kuweka mageti katika vyoo hiyo.

Pia  Anastazia Wambura  ametoa wito kwa Watanzania ambao ni watumiaji wa uwanja huo,kwa kuwataka kutumia vizuri miundo mbinu ya uwanja huo
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TING, Dk. Vernon Fernandes,ameelezea kile kilichomsukuma kutoa msaada huo,akisema ametoa msaada huo kwa kuwa kampuni hiyo inatambua kuwa kutoa ni moyo,na wao wametoa msaada huo kwa moyo mmoja.

Hata hivyo amewataka watanzania kutambua kuwa uwanja wa Taifa ni uwanja wao,na kuwataka waweze kuthamini uwanja huo.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments