Ticker

6/recent/ticker-posts

DRFA, KIFA WAITWA TFF

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 17,2016 SAA 12:46 JIONI
Mwenyekiti wa DRFA,Almasi Kasongo (Wpili kutoka kulia)
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu Uchaguzi wa Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa Kinondoni (KIFA) uliofanyika Juni 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam.

Kutokana na malalamiko hayo, TFF imewaita wagombea wote wa ngazi ya juu wa KIFA wakiwamo viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho kitakachofanyika kesho Jumamosi Juni 18, 2016 saa 3.00 asubuhi.

Pia, imewaita viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sambamba na Kamati za Uchaguzi za DRFA kadhalika ile ya KIFA ambazo zilisimamia uchaguzi huo ambao ulifanyika kwa mara ya pili mwishoni mwa wiki baada ya ule wa kwanza kuahirishwa mwezi uliopita.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments