TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzaia chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya
timu ya Shelisheli katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Kwanza kufuzu Fainali za U17 Afrika mwakani Madagascar.
timu ya Shelisheli katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Kwanza kufuzu Fainali za U17 Afrika mwakani Madagascar.
Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam,Serengeti Boys walitawala asilimia kubwa ya mchezo, na Mabao yao mawili yalipatikana katika kipindi cha kwanza,bao la
kwanza likipatikana katika dakika ya 15 likifungwa na Dickson Nickson Job.
Bao la pili la Serengeti Boys alifunga Ibrahim Abdallah Ali dakika ya 21 baada ya kuingiza mpira nyavuni uliotemwa na kipa Gino Pleursuse wa Seychelles (Shelisheli) ambaye alipigiwa shuti kali na Ally Hamis Ng'anzi.
Kikosi cha cha kwanza cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzaia chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoifunga 3-0 Shelisheli |
Kikosi cha kwanza cha Shelisheli |
Kipindi cha pili kilianza kwa Serengeti Boys kuonekana bado wakiutawala mchezo huo na katika dakika ya 14 mchezaji wa Seychelles (Shelisheli) aliunawa mpira katika eneo la Hatari na Refa kutoka Ethiopia Belay Tadesse Asserese kuamua penati ipigwe,na Ally Hussen Msengi akaweka nyavuni Penati hiyo dakika ya 15 na kuipatia Serengeti Boysbao la Tatu.
Mchezaji wa Serengeti Boys akimtoka beki wa shelisheli |
Mwanamuziki Lady Jaydee akiwa pamoja na meneja wake Seven Mosha wakishuhudia mchezo |
Serengeti Boys sasa inahitaji sare kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo dhidi ya Shelisheli ili kukata tiketi ya kwenda kukutana na Afrika Kusini.
0 Comments