Kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzaia chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoifunga 3-0 Shelisheli |
Siku ya Jumapili Jun.26 timu ya taifa ya vijana ya Tanzaia chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys ilifanikiwa kuibuka na ushindi
wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Shelisheli katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Kwanza kufuzu Fainali za U17 Afrika mwakani Madagascar.
wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Shelisheli katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Kwanza kufuzu Fainali za U17 Afrika mwakani Madagascar.
Serengeti Boys sasa inahitaji sare kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo dhidi ya Shelisheli ili kukata tiketi ya kwenda kukutana na Afrika Kusini.
Mara baada ya mchezo huo viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania Waliweza kuwapa maneno ya Busara vijana hao ambao walionesha soka la kuvutia katika mchezo huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye pamoja na Kocha mkuu wa Timu hiyo Bakari Shime waliweza kutoa maneno machache kwa wachezaji hao,lakini furaha na matumaini iliibuka kwa wachezaji hao mara baada ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania Jamal Malinzi kutoa ahadi (zawadi) kwa wachezaji hao endapo tu,Serengeti Boys itaitoa shelisheli katika mchezo wa marudiano.
Ni ahadi ipi ametoa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania Jamal Malinzi ?,sikiliza hapo chini.
SIKILIZA AHADI YA MALINZI
Katika
mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
salaam,Serengeti Boys walitawala asilimia kubwa ya mchezo, na Mabao yao
mawili yalipatikana katika kipindi cha kwanza,bao la
kwanza likipatikana katika dakika ya 15 likifungwa na Dickson Nickson Job.
Bao la pili la Serengeti Boys alifunga
Ibrahim Abdallah Ali dakika ya 21 baada ya kuingiza mpira nyavuni
uliotemwa na kipa Gino Pleursuse wa Seychelles (Shelisheli) ambaye
alipigiwa shuti kali na Ally Hamis Ng'anzi.
Kipindi cha pili kilianza kwa Serengeti Boys kuonekana bado wakiutawala mchezo huo na
katika dakika ya 14 mchezaji wa Seychelles (Shelisheli) aliunawa mpira
katika eneo la Hatari na Refa kutoka Ethiopia Belay Tadesse Asserese
kuamua penati ipigwe,na Ally Hussen Msengi akaweka nyavuni Penati hiyo
dakika ya 15 na kuipatia Serengeti Boysbao la Tatu.
0 Comments