Ticker

6/recent/ticker-posts

MADAM RITA KAJA NA KIPINDI CHA TV 'RITA PAULSEN SHOW ',LIVE AZAM TWO KILA JUMAPILI (PICHA/AUDIO)

   Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 10,2016 SAA 03:00 USIKU
Azama Tv kwa kushirikiana na BenchMark Prouction 360 Imezindua kipindi chake kipya cha Rita Paulsen Show
Kitakachoanza kuruka siku ya Jumapili Saa 1:00 Usiku kupitia Channel ya AzamTwo Inayopatikana kwenye Vifurushi Vya AzamTv.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Azam TV, Tido Mhando akizungumza na Waandishi wa Habari studio za kampuni hiyo, Tabata mjini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kipindi cha Rita Poulsen Show.
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa AzamTv Tido Mhando Amesema Kuwa kipindi hiki kimekuja wakati muafaka kikitoa majibu ya mpango mkakati ambao AzamTv imekuwa ikifanyia kazi maoni ya watazamaji wake kwa kuwaletea vipindi bora vinavyoelimisha na vyenye maudhui anayofaa kutazamwa na familia nzima.
Naye Muasisi wa Bench Mark Production na mtangazaji wa kipindi hicho Rita Paulsen ama maarufu kama Madam Rita alifunguka kwa kuelezea namna kipindi hicho kitakavyokuwa ni cha kipekee kwani kitabeba mijadala iliyofanyiwa uchambuzi wa kina na hadhi yake ni ya kimataifa na kitaifa na kitawafanya watazamaji wasibanduke hata KUPEPESA MACHO pembeni kuanzai mwanzo hadi mwisho kutokana na uhondo wake.

Rita alisema kuwa "Safari ya kufikia hapa haikuwa kazi rahisi hata kidogo kutokana na majaribu tuliyokutana nayo ya kuandaa kitu chenye ubora huu,na naweza kuthubutu kusema kuwa huyu ni 'Mtoto' wa kipekee kwa Benchimark Prodactio na ambaye amekuwa akisukwa kuanzia mwaka 2007 na tumekuwa tukihaha kupata mahala sahihi ambapo wataweza kumnyanyua 'Mtoto' huyu kwa hadhi yake anayostahili na hatimaye AzamTv pekee wameona umuhimu na thamani yake na kutupatia nafasi hii adhimu ya kufanya nao kazi ambapo leo tunazindua Rasmi"

Lengo kuu la Rita Paulsen Show ni kuelimisha,kuburudisha na kugusa maisha ya watu na kurudisha imani ya ubinadamu na matumaini ya maisha ambapo wageni mbalimbali wataalikwa wakiwemo watu maarufu,wenye historia ya pekee na hata wa kawaida watakaofunguka juu ya mapambano na visa vya maisha yao waliyopitia hadi kufikia kwenye mafanikio waliyonayo sasa.
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa AzamTv Tido Mhando nae alingeza kuwa 'kipindi hiki kitagusa hisia za watu kwani zitamuweka mtazamaji katika nafasi ile aliyekuwa nayo muhusika na kuelewa ni vipi na kwa nini alichukua maamuzi magumu,ya kugofya ya kusikitika na hata kufurahisha pia yatakayowaacha midomo wazi,mioyo iliyoumia na macho yaliyojaa machozi kutokana na msisimoko wake"

SIKILIZA HAPA
KKama ilivyo jina la kipindi Rita Paulsen ni mwanamke aliyetawala ulingo wa vipindi vya burudani kwa muda mrefu sasa na imekuwa ni ndoto yake kubwa kutumia nafasi yake na nguvu zake ndani ya nchi hata Afrika kuleta mabadiliko kwenye maisha ya watu,na kupitia kipindi chake hiki watazamaji wataweza kumuona kivingine akigusa maisha ya watu kiuchumi,kijamii,kiimani na hata kimwili na kuwarudishia imani waliyopoteza juu ya maisha.

Rita Paulsen Show ni kipindi cha dakika 45 kilichogawanyika katika sehemu kuu tatu,kitaruka kila Jumapili Saa 1:00 Usiku na marudio ni Alhamis saa 12:00 Jioni kupitia channel ya AzamTwo Ndani ya Azam Tv Pekee.

Utashuhudia simulizi za nguvu za mwanamke aliyetelekezwa,na watu maarufu wakifanya vitu ambavyo hukuvitegemea na kitakuacha na ile hisia ya kujisikia vizuri mwanzo mwisho.

ANGALIA PICHA ZAIDI
Kutoka kulia ni Tido Mhando, Rita Poulsen na Mkuu wa Idara ya Masoko ua Azam Media Limited, Mgope Kiwanga
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments