Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:YUSUFU MANJI NA MAKAMU WAKE SANGA WAMWAGA SERA ZAO...>>>...wasikilize hapa

   Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 10,2016 SAA 01:51 USIKU
Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans wanaomaliza kipindi cha uongozi ndani ya klabu hiyo,  
Yusuf manji pamoja na Clement Sanga hii leo wametoa shukrani kwa wanachama wa klabu hiyo ambao waliwachagua na kuwaingiza madarakani mwaka 2012.

Wawili hao wamefika mbele ya wanachama wa Young Africans katika mkutano maalum uliofanyika kwenye uwanja wa Kaunda jijini Dar es salaam kwa dhumuni la kutoa shukurani zao, sambamba na kuomba kura kwa mara nyingine ili waweze kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka minne ijayo.

Mwenyekiti wa Young Africans Yusuf Manji, amesema katika kipindi alichokaa madarakani yapo mambo mengi aliyoyafanya ikiwa ni pamoja na kuifikisha mbali klabu hiyo ambayo kwa sasa ni sehemu ya timu nane zinazoshiriki hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Manji ametumia nafasi hiyo kuwambusha wanachama waliokua wamehudhuria katika uwanja wa Kaunda jijini Dar es salaam juu ya ahadi yake ya kujenga uwanja wa kisasa endapo atapewa nafasi ya kuendelea kuiongoza klabu hiyo.

Naye makamu mwenyekiti Clement Sanga amewataka wanachama wa Young Africans kutokusisa kuwachagua tena, ili kukamilisha mipango ya kuifikisha klabu hiyo katika kilele cha uchumi.

SIKILIZA HAPA
KKWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments