Sakata la klabu bingwa Tanzania bara Young Africans la kushindwa kutumia jezi zao zilizozoeleka katika mchezo wa
kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejaia limechukua sura mpya, baada ya shirikisho al soka nchini TFF kuhusishwa.
Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa Young Africans Jerry Muro amesema shirikisho la soka nchini TFF lilikua linafahamu fika kilichokua kikiendendea baada ya kutumiwa taarifa na CAF lakini waliamua kunyamaza pasi na kuwaambia lolote.
Muro amesema mbali na kulikalia kimya jambo hilo, pia TFF wameshindwa kuwakabidhi kwa wakati vifaa vya mazoezi ambavyo vilitumwa kutoka CAF kwa anuwani ya shirikisho hilo la soka hapa nchini.
Kufutia tuhuma hizo Jamii na michezo imezungumza na Jerry Muro pamoja na afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Alfred Lucas , ili kujua kama kweli walifahamu suala la matumizi ya jezi ambazo Young Africans walipaswa kuzitumia wakati wa mchezo wao dhidi ya Mo Beijaia pamoja na kutumwa kwa vifaa vyao vya mazoezi kutoka CAF.
SIKILIZA HAPA
0 Comments