Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:REFA WA SIMBA 5 - 0 YANGA AOMBA UONGOZI JANGWANI,msikilize hapa

   Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 9,2016 SAA 05:45 USIKU
Mwamuzi aliyechezesha mchezo  wa SIMBA 5 - 0 YANGA  , Hashim Abdallah, akimpa kadi ya njano aliyekuwa golikipa wa timu ya Yanga, Said Kasalama katika mchezo huo baada ya kumdondosha Emmanuel Okwi alipokuwa ndani ya eneo la penalti na kisha kupigiwa adhabu hiyo, iliyopigwa na marehemu Patrick Mafisango na kufanya Simba hadi wakati huo kuongoza kwa mabao 3-0.
Wanachama wa klabu ya Young Africans waliopitishwa katika mchakato wa kugombea nafasi za uongozi wa klabu hiyo,
wameendelea na zoezi la kampeni dhidi ya wanachama wenzao ili kushawishi mpango wa kupigiwa kura.

Mgombea aliyepata nafasi ya kuzungumza na Jamii na Michezo ni muamuzi mstaafu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Hashim Mudhihir Abdallah ambapo amesema dhumuni kubwa la kujitokeza kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ni kutaka kusaidia kati ya maendeleo wa soka ya  klabu ya Young Africans.

Hashim ambaye alichezesha mtanange wa Simba na young Africans uliomalizika kwa mnyama kuibuka na ushindi wa mabao matano kwa sifuri mwaka 2012, amesema mbali na dhana hiyo pia ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa katika suala la ujenzi wa uwanja wa Kaunda.
 
 Mpaka dakika inayoonekana kwenye ubao wa matokeo, mabao yalikuwa kama inavyosomeka kwenye ubao huo.

 Mashabiki wa Yanga wakiwa wameshikwa na butwaa baada ya kufungwa goli la tano na Felix Sunzu.
Mashabiki wa Simba wakishangilia goli la pili la timu hiyo dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam 

MSIKILIZE HAPA

PICHA NA:wwwbayanablogspotcom.blogspot.com

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments