Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO: JERRY MURRO AFUNGUKA JUU YA JEZI MPYA,MECHI YA MAZEMBE NA TAARIFA ZA SIMBA SC KUMZUIA HASSAN KESSY

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 20,2016 SAA 01:34 USIKU
Mabingwa Tanzania bara Dar es salaam Young Africans wanatarajiwa kurejea nchini wakati wowote kuanzia kesho tayari
kwa maandalizi ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika CAF.

Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu hiyo iliyosalia kwenye michuano ya kimataifa katika ukanda wa Afrika mashariki, Jerry Murro amesema kikosi chao kitaweka kambi hapa nchini kutokana na hali ya hewa ya nchini Uturuki kutofautiana na ya hapa nchini ambapo mchezo wa pili dhidi ya TP Mazembe utakapochezwa.

Muro pia amezungumzi mchezo wa jana waliocheza dhidi ya Mo Bejaia na kushuhudia wakibamizwa bao moja kwa sifuri.
SIKILIZA HAPA

KKatika hatua nyingine Jerry Muro ametoa ufafanuzi wa suala la jezi zilizotumiwa na kikosi chao ambalo jana lilizua taharuki miongoni mwa mashabiki na wanachama, kutokana na kukosa sifa ya kutokuwepo kwa nembo ya mdhamini wao sehemu za kifuani.
Hata hivyo Jerry Muro amesema huenda kukawa na uwezekano wa kikosi chao kuvaa jezi zenye mdhamini tofauti na sasa, kufutia mkataba kati yao na kampuni hiyo kufikia kikomo.

Wakati huo huo Muro amerusha dongo kwa wapinzani wao jadi Simba ambao walizuia beki wa pembeni wa Hassn Kessy kutokucheza mchezo wa jana baada ya kuwasilisha barua kwenye makao ya shirikisho la soka barani Afrika CAF, kwa madai ya kuwa na mkataba na mchezaji huyo ambaye alijiunga na Young Africans mwishoni mwa mwezi uliopita.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments