Kampuni ya Azam Media imeingia makubaliano ya kimkataba na shirikisho la soka nchini TFF ya kuonyesha michezo ya ligi kuu ya
soka kwa wanawake ambayo itaanza rasmi mwezi August mwaka huu.
soka kwa wanawake ambayo itaanza rasmi mwezi August mwaka huu.
Makubalino ya pande hizo mbili yamesainiwa hii leo jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na waandishi wa habari, ambapo dhumuni kubwa ni kutaka kuendeleza soka la wanawake ambalo kwa muda mrefu limekua likidumaa kwa kukosa udhamini kama ilivyo kwa timu za wanaume.
Rais wa TFF Jamal Malinzi amesema tayari maandalizi ya kuchezwa kwa ligi hiyo yameshaanza na wamefanya maamuzi magumu ya kutoa nafasi kumi za upendeleo kwa timu shiriki.
Hata hivyo Malinzi amesema sehemu ya makubalino waliyoingia na Azam Media pamoja na kanuni za kuendesha ligi hiyo ya taifa ya wanawake, ni kuhakikuisha wahusika wanakuwa wasimamizi wakuu kwa lengo la kuendeleza Nyanja nyingine.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha soka la wanawake nchini TWFA, Amina Karuma ameyoa wito kwa wanawake nchini kote kuhakikisha wanautendea haki mkataba ulioingiwa hii leo kati ya TFF pamoja na Azam Media, kwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye harakati za kuendeleza soka kwa wasichana.
Wakati huo huo Jamal Malinzi ameweka hadharani makubaliano mengine ya kimkataba waliyofikia na uongozi wa Azam Media, kuhusu michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (Uhai Cup).
Malinzi amesema sehemu ya makubaliano waliyosaini hii leo ni kubadilihwa kwa mfumo wa michuano hiyo na sasa itachezwa kwenye mfumo wa ligi kama itakavyokua kwa timu za wakubwa, huku lengo linalodhamiriwa ni kuendeleza kupata vijana ambao watakuwa na sababu ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.
Mkataba wa michuano hiyo iliyosainiwa hii lao kati ya TFF pamoja na Azam Medea unathamani ya shilingi billion mbili (billion moja kwa wanawake na billion moja kwa vijana) na utadumu kwa miaka mitano.

0 Comments