Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:WAZEE WA YANGA WAZUNGUMZA JUU KUTENGWA KWA BAADHI YA WANACHAMA...sikiliza hapa...


Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.28,2016 SAA 01:40 USIKU

Uchaguzi wa klabu bingwa Tanzania bara, Young Africans huenda ukaingia dosari kutokana na hali ya sintofahamu iliyoibuliwa na
baraza la wazee wa klabu hiyo kuibua hoja ya kutengwa kwa baadhi ya wanachama katika zoezi ka kupiga kura ya kuwachagua viongozi wapya katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi ujao.
Katibu mkuu wa baraza la wazee wa Young Africans, Ibrahim Akilimali
Katibu mkuu wa baraza la wazee wa Young Africans, Ibrahim Akilimali hii leo alikutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es salaam na kueleza wasiwasi wa kuibuka kwa hali ya kutengwa kwa baadhi ya wanachama wakati wa zoezi la kupiga kura.


Wakati huo huo Ibrahim akilimali akawasilisha salamu kwa baadhi ya wanachama wa Young Africans ambao wanadhaniwa huenda wanataka kuibua vurugu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, kwa kuwaambia wasahau kutimiza malengo wanayoyakusudia.


MSIKILIZA MZEE AKILIMALI HAPA
KKWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments