![]() |
| Jamali Malinzi (katikati) kulia ni Raisi wa chama cha mpira Zanzibar Ravia Idarous Faina |
Kozi ya makocha wa CAF ya Leseni B iliyokua ifanyike kwa muda wa wiki tatu mwezi Septemba mwaka huu kisiwani
Zanzibar sasa imefutwa kufuatia kupeleka mpira mahakamani.
Sasa kozi hiyo itafanyika tena pindi kesi ya mpira itakapoondelewa mahakamani. Kumekua na hali ya kutokuelewana kwa uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kisiwani Zanzibar (ZFA) hali iliyopelekea uongozi wa ZFA kupelekwa mahakamani.
Kwa mujibu wa kanuni za FIFA, masuala ya mpira wa miguu hayapaswi kupelekwa mahakamani.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

0 Comments