Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA YA SIMBA KURUDI TENA ZANZIBAR

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.20,2015 SAA 02:04 USIKU
Katika matayarisho ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara, klabu ya Simba inatarajia
kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu 2015/2016.
Tovuti rasmi ya Simba imeongea na kocha msaidizi wa Simba Suleiman Matola na kusema “ni kweli tunatarajia kurudi tena visiwani Zanzibar kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mwisho kujitayarisha na ligi kuu Tanzania bara, ndani ya kipindi kifupi tutawaambia mashabiki na wanachama wa Simba kuwa ni lini tutaondoka kwenda Zanzibar”.
Rais wa Simba Evans Aveva siku ya Simba Day
"Tunarudi tena visiwani Zanzibar kwani kama vile unavyoijua Zanzibar ni sehemu tulivu sana na hata hali yake ya hewa ni hali rafiki kwa ajili ya mazoezi kwa wachezaji, ndio maana uongozi umeafiki sula la kikosi cha Simba kuweza kurudi tana Zanzibar kwa maandalizi ya Mwisho", Alisema Matola.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments