Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA YASAJILI KIUNGO WA KIMATAIFA TOKA ZIMBABWE.

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.1,2015 SAA 12:04 JIONI

Simba Sports Club (SSC) imeendelea na mkakati wa kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.
Katika muendelezo huo imemsajili kiungo wa kimataifa Justine Majabvi akitokea katika timu ya Vicem Hai Phong F.C nchini Vietnam pia alikuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Zimbabwe. Majabvi amewahi kuwa mwanasoka bora wa Zimbabwe mwaka 2005, 2007 na mwaka 2008. Kati ya mwaka 2008 – 2009 Majabvi alichezea timu ya Lask Linz FC ya Austria pia amewahi kucheza nchini Ujerumani kabla ya kuchezea Vicem Hai Phong F.C nchini Vietnam.
Taarifa katika Tovuti rasmi ya Simba inasema Kiungo Huyu wa kimataifa tayari amewasili Tanzania na kujiunga na Kambi Zanzibar. Wapenzi na wanachama wa Simba watapata fursa ya kumwona uwanjani siku ya Simba Day 8 August 2015.
Majabvi alizaliwa tarehe 26 – 3 – 1984 Harare Zimbabwe aliwahi kuicheza Klabu ya Lancashire Steel F.C ya nchini Zimbabwe mwaka 2002 – 2005, Dynamos Football Club (Dynamos Harare) ya nchini Zimbabwe mwaka 2006 – 2008 na Khatoco Khánh Hoà ya nchini Vietnam mwaka 2012.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments