Mshambuliaji Paul Mungai Kiongera alifunga mabao matatu peke yake hat-trick kwa timu yake ya Kenya Commercial Bank( KCB
) wakiishinda Thika United mabao 3-2 katika ,mchezo muhimu wa Ligi Kuu ya Kenya uliopigwa katika Uwanja wa Thika wa Manispaa weekend hii iliyopita siku ya Jumamosi.
Kenya Commercial Bank wamekuwa wakipambana kukwepa kushuka daraja, mchezo huo uliwapeleka juu kwa pointi 20 baada ya kucheza mechi 21.
Mshambulizi huo alifunguliwa akaunti yake katika dakika ya 20 kwa penalti kabla ya kuongeza la pili katika dakika ya 37. Kisha kukamilisha kwa mabao yake matatu dakika ya nane baada ya muda wa ziada wa mechi kumalizika.
Paul Mungai Kiongera alijiunga tena na kikosi chake hicho cha zamani akitokea katika klabu ya simba ya Tanzania,hata hivyo kwa mujibu wa makubaliano ni kwamba Simba ya Tanzania inaweza kumrejesha mshambuliaji huyo,mara baada ya miezi sita kukamilika.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments