Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:ANGALIA AZAM FC ILIVYO FURAHI NA UBINGWA BAADA YA KUICHAPA GOR MAHIA

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.3,2015 SAA 12:36 USIKU
Siku ya Jana klabu ya Azam FC iliweka historia baada ya kuchukua ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagame kwa
mara ya kwanza.




Azam Fc imetwaa ubingwa wa kimataifa wa CECAFA Kagame Cup kwa kucheza mechi sita za mashindano na timu mabingwa bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Uongozi wa Azam FC umethibitisha kwa vitendo kuwa haukukosea kumrejesha Kocha Muingereza Stewart Hall klabuni baada ya kukaa nje ya klabu kwa miezi 13 kwani miezi miwili tuu baada ya kutua amewezesha klabu kutwaa kikombe kikubwa baada ya kuwachapa Gor Mahia ya Kenya bao 2-0.











Mabao hayo yaliyowapa heshima Azam FC yalipachikwa dakika ya 16 na nahodha John Bocco (Boko Haram) aliyeunganisha krosi safi ya Muivory Coast Kipre Tchetche na la pili lilimaliziwa na Tchetche dakika ya 65 kwa njia ya faulo iliyokwenda moja kwa moja golini na kumshinda kipa wa Gor Boniface Oluoch.

ANGALIA PICHA 


























KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments