1.Taarifa ya kwanza ni ya Katibu mkuu wa baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA, Nicolas
Musonye amegusia mahala ambapo wanatarajia michuano ya Kombe la Kagame itachezwa kwa mwaka 2016, huku akionyesha kuipa nafasi nyingine nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji kwa kuutazama upande wa pili wa muungano wa Tanzania.
2.Mipango ya timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, kwenda kuweka kambi visiwani Zanzibar imeingia gizani kufuatia shirikisho la soka nchini TFF kupokea taarifa za kukosekana kwa uwanja wa kufanyia mazoezi kwa timu hiyo.
kocha mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage amezungumza kuhusu ishu hiyo.
3.Aishi Manura kipa wa Azama Fc amezungumza na Jamii na Michezo na kuelezea jitihada zake katika michuano ya kombe la Kagame,na kumaliza bila ya kuruhusu hata bao moja.
4.Kocha mkuu wa klabu ya Dar es salaam Young Africans, Hans Van De Pluijm, ametoa sababu ya kikosi chake kushindwa kutimiza lengo la kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la Kagame iliyomalizika jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma lililopita.
5.Simba Sc wako Zanzibal na hii leo Kocha Msaidizi wa Simba Sc SULEIMAN Abdallah Matola Ameelezea maendeleo ya Kambi yao.
KIMATAIFA
Mshambuliaji wa Simba Paul Mungai Kiongera alifunga mabao matatu peke yake hat-trick kwa timu yake anayocheza sasa ya Kenya Commercial Bank( KCB) wakiishinda Thika United .
Klabu ya Lyon ya Ufaransa imemsajili beki wa kulia wa Manchester United Rafael da Silva kwa mkataba wa miaka minne na kwa kitita ambacho hakikutajwa.
SIKILIZA HAPO CHINI

0 Comments