Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:STARS YAJIFUA TENA LEO,WENYEJI ETHIOPIA WATAKA KUPIMANA NGUVU

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 6,2015 SAA 09:02 MCHANA
Displaying thumb_IMG_2091_1024.jpg
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, leo kimeendelea na
mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Jana kikosi cha Stars kilifanya mazoezi majira ya saa 9 mchana katika uwanja wa Taifa wa Ethiopia (Addis Ababa) ambao pia unatumiwa na timu yao ya Taifa kwa mazoezi.
Displaying thumb_IMG_2131_1024.jpg
Displaying thumb_IMG_2127_1024.jpg
Displaying thumb_IMG_2129_1024.jpg
Displaying thumb_IMG_2120_1024.jpg
Taifa Stars ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Misri.

Daktari wa Taifa Stars, Billy Haonga amesema hali ya hewa ya Addis Ababa ni nzuri kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri, kutokana na timu kufanya mazoezi katika ukanda wa juu (mwinuko kutoka usawa wa bahari) hali itakayopelekea wachezaji kuwa fit kwa ajili ya mchezo.

Hali ya hewa ya Alexandria ni ya kawaida, hakuna baridi sana kutokana na kuzungukwa na bahari ya la Mediterania, hivyo kipindi cha wiki moja tutakachokuwa kambini hapa Addis Ababa tunatarajiwa vijana watakua vizuri kabisa kw aajili ya mchezo” Alisema Haonga”.
Displaying thumb_IMG_2121_1024.jpg
Displaying thumb_IMG_2117_1024.jpg
Displaying thumb_IMG_2111_1024.jpg
Wachezaji wote wa Taifa Stars waliopo kambini Addis Ababa wapo katika hali nzuri, kiafya, kifikra na morali ya juu kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao. 

Wenyeji Chama cha Soka cha Ethiopia (EFF) wanaangalia uwezekano wa Taifa Stars kupata mchezo mmoja wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya kuelekea nchini Misri.
Displaying thumb_IMG_2110_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_2091_1024.jpgDisplaying thumb_IMG_2093_1024.jpg

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments