Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya COSAFA Castel Cup dhidi
ya timu ya Taifa ya Swaziland, baada ya kufungwa bao 1- 0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.
Stars ilipoteza nafasi zaidi ya tano kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wake Saimon Msuva na nahodha John Bocco ambao walishindwa kukwamisha mpira wavuni katika kipindi cha kwanza, ambacho Taifa Stars ilicheza vizuri.
Swaziland walipata bao lao la kwanza na la ushindi dakika ya 42 ya mchezo, kupitia kwa mlinzi wa kulia Sifiso Mabila aliyepanda kuongeza nguvu ya mashambulizi na kuachia shuti lililouacha mlinda mlango wa Stars akikosa cha kufanya kuokoa mchomo huo.
Kipindi cha pili Stars walizidiwa kwani mashambulizi yao hayakua na madhara langoni mwa Swaziland na kumuacha mlinda mlango Mphikeleli Dlamnini akiwa likizo kwa muda mrefu.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments