Siku ya leo Jumanne kuna mchezo mmoja wa ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich dhidi ya Barcelona,ambapo mchezo huo
ni nusu fainali ya pili baada ya mechi ya awali Bayern Munich kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa timu ya Barcelona.
Kuelekea katika mchezo huo Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola ,anasema Bayern Munich lazima wawe na subira wakati timu hiyo itakapo jaribu kugeuza matokeo hayo ya 3-0 dhidi ya Barca.
Guardiola ambaye pia amekanusha taarifa za kujiunga na Manchester City akisema bado ana Mkataba wa mwaka mmoja zaidi na Bayern Munich,anasisitiza Bayern lazima wawe waangalifu katika mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Allianz Arena au kuweza kukabiliana na mashambulizi ya Messi, Neymar na Luis Suarez.
"Sisi tuko nyuma kwa mabao 3-0 dhidi ya timu yao, timu bora Ulaya miaka 15-20 iliyopita," alisema Guardiola, ambaye alishinda mataji 14 katika kipindi cha miaka minne kama kocha wa Barca hadi mwaka 2012.
Pep Guardiola amesema watajilinda katika mchezo wa leo.na anajua jinsi watu wa nchini Ujerumani wanavyofikiri. Lakini amesisitiza timu yake itajilinda na kusonga mbele,
kwa sababu Barca ina wachezaji imara na washambuliaji bora.
Awali Pep Guardiola alikataa kuwapa lawama yoyote wachezaji wake wa Bayern Munich licha kushuhudia timu yake ikiangamia kwa kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Barcelona katika dimba la Nou Camp,mchezo wa nusu fainali ya kwanza.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments